Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi

Jukwaa la Huduma ya Rasilimali ya Nidhamu ya Kisiasa Lazinduliwa Rasmi katika Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU)


15 October 2021 | By 褚予钦 Jamila | SISU

Ili kuimarisha msaada kwa ufundishaji na utafiti wa taaluma shuleni, na kutoa huduma za rasilimali ya habari za kitaalam zaidi tena zinazolengwa kwa walimu na wanafunzi wa taaluma tofauti, maktaba ya shule imefanya uchunguzi na majaribio ya ujenzi wa jukwaa la huduma ya rasilimali ya nidhamu. Baada ya kujadili na idara husika katika hatua ya mwanzo, na kwa msingi wa uchunguzi wa kina wa mahitaji ya rasilimali ya habari ya nidhamu ya kisiasa, maktaba imejenga “Jukwaa la Huduma ya Rasilimali ya Nidhamu ya Kisiasa”. Jukwaa limebuniwa na kujengwa kulingana na dhana ya huduma zenye usahihi na maridadi. Linachagua kwa uangalifu na kukusanya rasilimali ya habari zinazotumiwa sana na zenye mamlaka ya masomo ya kisiasa, na linaunganisha ujuaji wa habari na utafiti wa kisayansi. Inaweza kutoa huduma za kibinafsi na za kitaalam ili likidhi mahitaji ya ufundishaji na utafiti wa kisayansi. Siku chache zilizopita, Jukwaa la Huduma ya Rasilimali ya Nidhamu ya Kisiasa limezinduliwa rasmi kwenye ukurasa wa kwanza wa maktaba ya shule.

Jukwaa la Huduma ya Rasilimali ya Nidhamu ya Kisiasa la SISU ni jukwaa pana linalounganisha rasilimali za masomo, habari, na msaada wa utafiti wa kisayansi. Jukwaa limegawanywa katika makusudi nne ya kazi: 

Kwanza, Rasilimali ya Masomo inajumuisha aina mbalimbali za rasilimali za kitaaluma na matokeo ya utafiti katika uwanja wa Sayansi ya Kisiasa, ambayo inafunika aina kuu za rasilimali ya habari kama vile vitabu, majarida, na tasnifu. Inaweza kutoa marejeo ya utafiti wa masomo kwa “hatua moja”.

Pili, Vitabu vya Elektroniki vya Kufundisha inajumuisha vitabu vikuu vya kufundishia kwa kozi za Sayansi ya Kisiasa, ambvyo vinaweza kukidhi mahitaji ya vitabu vya elektroniki kwa ufundishaji wa kozi, hasa kwa masomo kwa njia ya mtandao.

Tatu, Misaada ya Habari & Utafiti inatoa miongozo ya uwasilishaji kwa majarida ya CSSCI na SSCI katika Sayansi ya Kisiasa, tena inatoa rasilimali ya “Kozi Ndogo” za ujuaji wa habari kama vile marejeo ya habari, uandishi wa insha, maadili ya taaluma, kanuni za kitaaluma na zana za utafiti n.k. Sekta hii inasaidia walimu na wanafunzi kufaulu jinsi ya kupata habari kwa ufanisi na ujuzi wa kuandika insha.

Nne, Maonyesho ya Mafanikio inaonyesha matokeo ya utafiti wa Sayansi ya Kisiasa shuleni, na kutoa takwimu za rasilimali ya masomo, n.k.

Jukwaa la Huduma ya Rasilimali ya Nidhamu ya Kisiasa ni jukwaa jingine mpya la huduma ya mada iliyoundwa na maktaba baada ya Bandari ya Habari za Nidhamu ya Usimamizi wa Biashara ijengwe. Pia ni uvumbuzi mpya wa maktaba kusaidia maendeleo ya masomo na kutoa huduma bora za ujuzi kwa nidhamu tofauti. Mfano wa jukwaa la masomo utakuwa na athari kubwa zaidi kwa kutumikia taaluma zaidi katika shule nzima. Siku zijazo, maktaba itaendelea kushirikiana na shule na idara zinazohusika ili kuendelea ujenzi wa majukwaa ya rasilimali zaidi ya habari inayolingana na mahitaji ya taaluma tofauti, na kukidhi mahitaji ya rasilimali ya habari za kibinafsi za taaluma, tena kusaidia maendeleo thabiti ya ufundishaji na utafiti wa taaluma mbalimbali.

Gawanya:

Press Contact

SISU News Center, Office of Communications and Public Affairs

Tel : +86 (21) 3537 2378

Baruapepe : news@shisu.edu.cn

Anuani :550 Dalian Road (W), Shanghai 200083, China

Soma Zaidi