Loading...

Soma Zaidi

Burudani kwenye Msitu wa Mvua: uchunguza Hadithi na Uchawi wa Wenyeji wa Alangan nchini Ufilipino


Msemaji: Shi Yang

Wakati: 19:00-20:30, tarehe 16(Jumamosi), Aprili

Mahali: Tencent Meeting (ID:985-6087-8648)

Lugha: Kichina

 

Utangulizi

Asia Kusini-mashariki ni hazina anuwai za utamaduni wa wanadamu, bustani yenye burudani ya kufanya utafiti wa uwandani kwa wanachuoni wa mila na desturi ya jamii (folklorists) na wanaanthropolojia na uwanja mzuri kwa wasomi wa Kichina kujihusisha na utafiti wa makabila ya ng'ambo. Watu wa Alangan-Mangyan, wenyeji wa milimani katika sehemu ya kati ya Ufilipino, ni watu wasiojua kusoma na kuandika wanaoishi kwa kufyeka na kuchoma na ukulima wa kuhamahama. Isitoshe, watu hao wana mila nyingi simulizi na matambiko ya uchawi. Mhadhiri huyo amefanya utafiti wa uwandani miongoni mwao kabila hilo la kienyeji kwa mara nyingi, akisafiri kupitia milima na mito kwa zaidi ya miezi minane. Alipofanya utafiti wa uwandani katika vijiji vingi vya Alangan, alizingatia fomu za kuenea kwa hadithi, njia za imani na mambo mengi yanayohusiana kwa karibu na hekaya, kama vile uganga, mafumbo, uchawi na kadhalika. Msemaji ataanza kutoka utafiti wa uwandani, ataonyesha idadi kubwa ya picha zilizopigwa na yeye binafsi na kuzungumzia hadithi zenye furaha wakati wa kufanya utafiti wa uwandani. Kutokana na hizo, atatambulisha imani za wenyeji, hadithi na hekaya na utendaji wa uchawi, ili kuwawezesha wasikilizaji wapate uzoefu wa utamaduni tofauti katika msitu wa mvua wa kitropiki.

 

Utangulizi wa Msemaji

Shi Yang, daktari wa Fasihi na naibu profesa, ni mkurugenzi wa Idara ya Asia Kusini-Mashariki ya Kitivo cha Lugha za Kigeni katika Chuo Kikuu cha Beijing (PKU), pia ni msaidizi mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma ya Fasihi ya Mashariki ya PKU. Nyanja zake mkuu za utafiti ni pamoja na utamaduni wa kilugha wa Ufilipino, utamaduni wa kijamii na fasihi ya mitaa ya Asia Kusini-Mashariki.

Gawanya:
Loading...

Soma Zaidi