Loading...

Soma Zaidi

Umoja katika Uanuwai: Maonyesho ya Lugha za Umoja wa Ulaya (EU)


Wakati: tarehe 17, Septemba, mwaka 2021 (Ijumaa)

Saa: 15:30 p.m. (Shanghai) / 09:30 a.m. (Brussels)

Mahali: Ukumbi wa Mada Maalumu wa Makumbusho ya Lugha za Dunia, Kampasi ya Songjiang / ZOOM (kwenye mtandao)

Lugha: Kichina, Kiingereza

 

Maonyesho ya Lugha za Umoja wa Ulaya yanawaalika wageni kwa dhati kuanza safari ya maendeleo ya lugha za Umoja wa Ulaya, ili kufahamu jinsi dhana ya lugha ilivyochangia katika kukuza uvumilivu, kuimarisha mshikamano, na kuondoa ubaguzi na sehemu nyingine, na kueleza uongozi wa kauli ya Umoja wa Ulaya: “Umoja katika Uanuwai”.

Pamoja na nchi wanachama 27, watu milioni 450 hivi na lugha 24 za kikazi zinazohusika, Umoja wa Ulaya ni mfano hai wa lugha nyingi za utekelezi. Umoja wa Ulaya unawapa raia haki za kimsingi za kuwasiliana na taasisi za Umoja wa Ulaya kwa kutumia lugha za nchi zao, na sheria zote za Umoja wa Ulaya zimetafsiriwa katika lugha 24 rasmi, ili kuhakikisha zipatikane na watu wote. Chini ya uongozi wa dhana ya lugha nyingi, utamaduni maarufu, mila ya kijadi na rasilimali ya lugha za Umoja wa Ulaya zinaweza kuonyeshwa na kurithishwa.

Mara hii maonyesho ya mada maalumu yatarejea jinsi huduma za ukalimani na tafsiri zilizotolewa na Umoja wa Ulaya zilivyokuza dhana ya lugha nyingi, na pia kuonyesha picha kwamba huduma za lugha zinazotolewa na Umoja wa Ulaya zitaendelea vizuri na kuwa na mustakabali mzuri.

Ushirikiano baina ya DG SCIC (Directorates General for Interpretation and Translation) na China ulianza mwaka 1979, na pande zote mbili zilianzisha Mradi wa Kufundisha Tafsiri kwa Kichina na lugha za Ulaya katika mwaka 1985, ili kuwatoa maofisa vijana wa wizara za China mazoezi ya tafsiri kwa miezi mitano. Hadi leo, wanafunzi zaidi ya mia tano wamekwenda kusomea huko Brussels.

Mwishowe, tutaangalia changamoto na fursa zinazokabiliwa na sekta za tafsiri na ukalimani za kitaaluma katika siku za mbele, na kushuhudia pamoja huduma za lugha ziwe na sura mpya katika maendeleo ya utandawazi wa karne ya 21.

Gawanya:
Loading...

Soma Zaidi