Bendera ya SISU

NEMBO

SISU ina nembo iliyo sehemu kuu ya kitambulishi chake kwa picha. Katika nembo kuna herufi tatu za Kichina, kitabu kilicho wazi na matawi mawili ya mzeituni yanayozivingira. Matawi ya mzeituni ni ishara ya amani na urafiki na kitabu kinaashiria hamu ya ujuzi na ukweli. Herufi tatu za Kichina “上外”ni ufupisho wa Kichina wa jina la chuo kikuu. Pia kuna SISU – ufupisho wa jina la chuo kikuu kwa Kiingereza na 1949 mwaka wa kuanzishwa kwake.

Tangu mwanzo wake, SISU imekuwa ikijitolea kuendeleza mabadilishano ya kimataifa ya China, yaliyo kiini cha ujumbe wa SISU tangu mwanzo na wajibu wa kutekelezwa na wahitimu wa SISU.

Hivyo basi, nembo hii iliundwa kusimamia ujumbe na ahadi za SISU za kuyakuza mawasiliano ya kimataifa ya kubadilishana huku wahitimu wake wakiitumikia dunia yote.

MKARARA WA NEMBO

http://de.shisu.edu.cn/common-uploads/2014/12/up_14181148422661575_0.png

Mstari wa Kichina wa nembo ya chuo kikuu ulidondolewa kutoka kwenye kitabu cha Lu Xun cha hati-mchoro. Mstari huu umetumika tangu mwaka 1956 wakati chuo bado ni Taasisi ya lugha za Kigeni ya Shanghai (Shanghai Foreign Language Institute).

RANGI

Rangi ya kuwakilishia SISU ni samawati SISU (samawati ya bahari), ambayo inawakilisha moyo wa kuikumatia dunia kama vile bahari inavyoikaribisha mito.

Ringi kiufundi: rangi msingi – Pantone (pms) 2945 / CMYK (100, 50, 0, 10).

Lu Xun na SISU: Zaidi ya bustani

Lu Xun, mwanzilishi wa fasihi usasa ya Kichina, ana uhusiano wa kudumu na SISU kwa njia nyingi. Upande mwingine wa tawi la Hongkou, kuna bustani moja ambako  Lu Xun amezikwa. Hata ingawa inajulikana zaidi kuwa Lu Xun alikuwa mshauri, mwanamapinduzi na mwandishi hodari, kimsingi alikuwa ni mtafsiri na mtaalam wa isimu na lugha. Maisha yake kama mwanafasihi yalianzia na kumalizikia katika utafsiri. Umuhimu wa kazi zilizotafsiriwa naye kiidadi na kimaana, si tofauti na zile alizoziandika mwenyewe.

Oktoba 10, mwaka wa 1936 Lu Xun aliandika katika shajara yake: "... Wakati wa mchana mimi na Guangping [mkewe], Haiying [mtoto wake], Mali [mpwa wake] tulienda sinema ya Isis kuona Dubrovsky. Kisasa. Filamu nzuri sana."

Hii "filamu nzuri sana" aliyoitaja ilikuwa imetengenezwa kutokana na riwaya ya Alexander Pushkin na kutafsiriwa na Jiang Chunfang, mhadhiri mkuu wa kwanza wa SISU. Kuonyesha sinema hiyo pia kulikuwa mumeandaliwa na Jiang, ambaye alijawa furaha tele kumwona Lu Xun katika ukumbi wa sinema. Alimkabidhi kitabu cha picha za Alexander Pushkin cha maadhimisho ya miaka 100 tangia kifo chake. Alimweleza Lu Xun kwamba maelezo ya wasifu a Pushkin yaliyokuwa katika kitabu hicho cha picha yalikuwa  kazi yake katika Makala ya Yiwen (yaani tafsiri) – gazeti la kila mwezi ambalo lilihaririwa na Lu Xun.

Pia Jiang alimwambia Lu Xun kwamba hapo awali filamu ilikuwa imepewa jina kwa Kichina, yaani; “kisa cha mapenzi katika kisasi”, na jina la sasa lilikuwa matokeo ya jaribio la mamlaka Kuomintang la kuibadilisha. Lu Xun alitoa maoni yake kwa hasira akisema kwamba wanamamlaka walifanya hivyo ilimradi kuwakanganya watazamaji wasiweze kujua chochote kuihusu filamu kutokana jina lake. Kwa vile filamu ilikuwa yaanza, Jiang alimpokeza Lu Xun tiketi zingine mbili na akamkaribisha arudi. Kwa bahati mbaya, hii ndiyo iliyokuwa filamu ya mwisho ambayo Lu Xun aliitazama  maishani mwake.

Muda mfupi baada ya kuanzilishwa kwa Jamhuri ya Wananchi China mwaka 1949,  kwa ombi na usaidizi wa meya wa Shanghai Chen Yi, Jiang Chunfang alianzisha Shule ya Kirusi Shanghai ikiwa mshiriki wa Chuo Kikuu cha Mapinduzi cha Wananchi Mashariki ya China (East China People’s Revolution University) – hii ndiyo SISU ya leo.

Gawanya: